SAFARI LAGER YATANGAZA RASMI UPATIKANAJI WA FOMU ZA PROGAMU YA SAFARI LAGER WEZESHWA MSIMU IV

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi upatikanaji wa fomu za programu yake ya Safari Lager Wezeshwa kwa msimu wa nne kwa wajasiriamali wadogo wadogo na wa kati Nchini. Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa bia ya Safari Lager Bi. Edith Bebwa alifafanuwa ya kwamba “ Fomu za ushiriki zitapatikana kwenye mabohari ya TBL, Mawakali wa kusambaza bia, kwenye mtandao wa www.wezeshwa.co.tz .

Fomu hizo zichukuliwe, zijazwe na kurejeshwa kwenye vituo vilivyotajwa hapo juu au kwa njia ya posta kwa sanduku la posta (Safari Lager Wezeshwa msimu wa nne,Tbl Dar es Salaam,P.o Box 9393 DSM).

Alisema Bi Edith, hii ni hazina tosha kwa wajasiriamali wadogowadogo nchini kwani itarahisisha kazi kwa kuwepo na vitendea kazi bila ya kutumia nguvu nyingi”.

Programu hii ni msimu wa nne tangu kuanzishwa kwake na imeleta mafanikio makubwa kwa wajasiriamali waliopata uthubutu wa kujaribu kujiunga na hatimae kuongeza uchumi wa nchi.

Programu hii itafanyika takribani mikoa yote ambapo itawapa fursa wajasiriamali wa aina zote bila kujali fani,kabila wala jinsia kujaza fomu kwa usahihi na kamilifu kisha kuzirudisha mahala husika na baadae waliokidhi nafasi zinazohitajika kuchaguliwa kisha kupewa mafunzo mafupi pamoja na kukabidhiwa ruzuku zao alisema Bi Edith.

Meneja wa bia ya Safari Lager, Edith Bebwa alimaliza kwa kutaja tarehe ya mwisho wa kurejesha fomu kuwa ni 20,Februari 2015 hivyo wajasiliamali wanapochukua fomu wakumbuke pia muda wa kuzirejesha walipozitoa.

Nae kiongozi wa wataalamu wa ushauri wa biashara kutoka kampuni ya TAPBDS, Bwana Joseph Migunda alisema kuwa “Zoezi hili linahusisha wataalamu wenye uwezo na uzoefu mkubwa katika kushauri na kusaidia ukuzaji wa sekta ya biashara ndogo na kubwa.

Hivyo aliomba wajasiriamali wote kuitumia fursa hii kushiriki kwa kuzingatia vigezo vilivyoainishwa kwenye fomu ya ushiriki. Wenye nia ya kufika mbali kibiashara na wenye malengo ya kuisaidia jamii inayowazunguka wasisite kuchangamkia fursa hii”.
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati kutangaza upatikanaji wa fomu za kuomba ruzuku za wajasiliama kwa msimu wan ne wa program ya Safari Lager Wezeshwa uliofanyika Dar es Salaam jana.Kulia ni Jaji wa Programu hiyo, Joseph Migunda.

No comments:

Powered by Blogger.